Pichani ni vikombe sita (6) ambavyo Shule za Msingi Halmashauri ya Mji wa Makambako zimepata Katika zoezi zima la Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) kwa Ngazi ya MKoa wa Njombe,Mashindano hayo yalianza katika shule ya Msingi Makambako kwa kata zote zinazounda Halmashauri ya Mji wa Makambako na kufanya zoezi la upembuzi wa Wanafunzi wa kuiwakilisha Halmashauri ya Mji wa Makambako kwa ngazi ya Mkoa,Zoezi ambalo lilifanikiwa kupata Wanafunzi ambao waliibeba bendera ya Halmashauri ya Mji wa Makambako kwaajili ya kwenda kushindana kwa ngazi ya Mkoa.
Katika picha ni wafanyakazi na Wanafunzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako pamoja na vikombe ambavyo wamevipata katika UMITASHAMTA 2021 kwa ngazi ya Mkoa wa Njombe ambapo katika zoezi hilo Halmashauri ya Mji wa Makambako imefanikiwa kupeleka Wanafunzi Ishirini na Moja wa UMITASHUMTA Kwa ngazi ya Taifa huko Mkoani Mtwara ambako mashindano hayo yanafanyika kwa Mwaka huu.Katika picha ni Wanafunzi wakionesha ni namna gani wamepata vikombe sita na kuwa washindi kwa Halmashauri zote za Mkoa Wa Njombe,Mnamo tarehe moja June Wanafunzi hao katika Halmashauri ya Mji wa Makambako walipata wasaa wa kutumbuiza Michezo yao mbele ya kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambo ni kwa jinsi gani walifanikiwa kuibuka washindi,Je yaliyomo yamo?,kama wanavoonekana na Mavazi yao ya kitamaduni katika Picha,Wanafunzi hao wameonyesha machache ambayo yamefanya wao kuibuka washindi wa vikombe sita ,Na moja ya mchezo ambao ulioneshwa ni Ngoma ya asili ya kabila la Wabena inayoitwa ''Yuheyo.''
Akipokea vikombe hivyo Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Makambako Rashidi Njozi,Amesema ni jambo la kujivunia kwa ushindi mkubwa hasa kwa Walimu na Maafisa Utamaduni na Michezo waliojitoa kwa hali na mali kwaajili ya kuwafundisha watoto na kuwaanda kwaajili ya UMITASHUMTA 2021 "Ni seme tu ukweli waliowaandaa watoto wamejitahidi sana sio kazi Rahisi kuvitwaa vikombe sita peke yetu na kuziacha mbali Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe kwakweli mmetuwakilisha na mmeiwakilisha Halamshauri yetu kwa Moyo wote ,Nawapongeza sana alisema Njozi".Ameongeza kuwa kwa waliotoka katika Halmashauri yetu kwaajili ya kwenda UMITASHUMTA Kitaifa huko Mkoani Mtwara ni imani kubwa watafanya vizuri kutokana na maandalizi waliyopata kwa walimu pamoja na maafisa Tamaduni na Michezo tuwaombee kheri katika Mashindano hayo.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa