Na. Lina Sanga
Viongozi wa Serikali na chama Wilaya ya Njombe wametakiwa kushiriki na kusimamia zoezi la Sensa kukamilika ndani ya Muda uliopangwa ili kuijengea heshima Wilaya na Mkoa wa Njombe kwa ujumla.
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Njombe,Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa katika mkutano wa Viongozi wa chama, Madiwani, Wakuu wa idara na vitengo pamoja na Watendaji wa Kata na Mitaa wa Halmashauri ya Mji Makambako.
Mhe. Kissa amesema kuwa,Ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Samia Suluhu Hassani,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya awamu ya sita anayoiongoza,kila kiongozi katika wilaya ya Njombe kwa nafasi yake hana budi kuhakikisha zoezi la Sensa linafanikiwa kwa ufanisi ndani ha Muda uliopangwa.
Amesema kuwa kukosekana kwa posho si kigezo cha kiongozi yeyote kususia zoezi,kwani kwa kufanya hivyo ni kukwamisha utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kuisababishia Serikali hasara kwa kukosa takwimu sahihi za watu kwa ajili ya Maendeleo.
Ametoa wito kwa Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi kuhakikisha wananchi katika maeneo yao,wanaandaa taarifa zote muhimu zinazohitajika ili kuwarahisishia makarani kufanya kazi kwa muda mfupi kwa kila kaya.
Baadhi ya taarifa zinazohitajika ni pamoja na majina kamili ya kila mwana kaya,jinsia yake,umri,hali ya ndoa,nyaraka mbalimbali kama namba ya NIDA au kitambulisho cha NIDA,vyeti vya kuzaliwa ,bima za afya, kitambulisho cha mpiga kura,taarifa za elimu,taarifa za hali ya afya,taarifa za jmiliki wa ardhi,majengo,vifaa/rasilimali,taarifa za shughuli za kiuchumi na taarifa za vizazi na vifo katika kaya.
#Jiandaekuhesabiwa2022
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa