• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO
HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na maliasili
      • Raslimali watu na Utawala
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Usafi na mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Ujenzi na Uokoaji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Sekondari
      • Kilimo, Ushirika na umwagiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
    • Vitengo
      • Sheria
      • ICT and Public relations
      • Ugavi na Manunuzi
      • Mkaguzi wa ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti mbalimbali
    • Mikataba
    • Mpango Mkakati
    • Hatua
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio
    • jarida la mji

Waajiri na Watendaji acheni kutoza maombi ya Ukarani wa Sensa

Tarehe iliyowekwa: May 12th, 2022

Waajiri na watendaji wa Kata ,Mitaa na Vijiji wametakiwa kutopokea fedha kwa waombaji wa nafasi ya ukarani katika zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika agosti 23 mwaka huu Nchini kote kwani tabia hiyo haikubaliki.

Rai hiyo imetolewa leo na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi  Mwaka 2022,Mhe. Anna Makinda katika kikao kazi cha Maafisa habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kinachofanyika mkoani Tanga.

Mhe. Makinda amesema kuwa, wapo baadhi ya waajiri kutaka watumishi wao kutoa fedha ili wapitishe maombi yao sambamba na watendaji kutaka malipo ili kugonga mihuri katika fomu za maombi ya ukarani wa sensa.

Ametoa angalizo kwa wananchi na watumishi wote wenye nia ya kuomba kazi ya ukarani wa sensa kutotoa fedha yoyote ili kupata kazi ya sensa,kwani maombi hayo yanapokelewa kupitia mtandao na sio ana kwa ana, ili kupata watu wenye uwezo na sifa na sio kwa kigezo cha undugu au kufahamiana.

Aidha,amesema kuwa maandalizi ya sensa hadi sasa yamekamilika  kwa asilimia 81,hivyo wananchi wajiandae kuhesabiwa ili kupata takwimu sahihi za watu na majengo yaliyopo nchini.

"Sensa ya mwaka huu ina sehemu kuu mbili,sehemu ya Sensa ya watu na sehemu ya Sensa ya majengo, ambayo kwa mara ya kwanza    inafanyika nchini mwaka huu  ili kutambua idadi ya majengo yaliyopo nchini na matumizi yake ili kuwezesha Serikali katika sera ya ardhi",alisema Makinda.

Nafasi za ukarani wa sensa ni karani wa kuhesabu watu,karani wa usimamizi wa maudhui na karani wasimamizi wa TEHAMA na sifa kuu ya mwombaji wa nafasi hizo ni pamoja na uwezo wa kutumia Simu janja kwani Sensa ya mwaka huu itatumia TEHAMA tofauti na sensa zilizopita.

Matangazo

  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 13 April 19, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 12. April 20, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 11. April 21, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 10. April 22, 2025
  • Fungua

Habari Mpya

  • Wataalamu na viongozi watakiwa kusimamia upatikanaji na utoaji wa huduma za chanjo.

    April 25, 2025
  • Makambako yang'ara katika tuzo za Afya ya Usafi wa Mazingira ngazi ya Halmashauri za Miji.

    April 09, 2025
  • Jumla ya Miti 15,000 kupandwa Halmashauri ya Mji Makambako kuelekea siku ya Miti duniani mwaka 2025.

    March 15, 2025
  • Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 2025 Mkoa wa Njombe, Mila kandamizi zaelezwa kuwa kikwazo cha ustawi na uwezeshaji

    March 09, 2025
  • Fungua

Video

Shule mpya ya Mbugani Kitandililo sekondari kupitia mradi wa SEQUIP
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Fursa za Usafirishaji
  • Orodha ya Madiwani
  • Uzalishaji wa Umeme wa Upepo
  • Organisation Structure
  • Fursa za Biashara
  • By Laws
  • Permanent Committee

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu ya Rais
  • Tovuti ya Ofisi ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Open Data Tanzania

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Makambako Town Council

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako

    Simu ya mezani: 026-2730044

    Simu ya Kiganjani: 0785635383

    Barua pepe: td@makambakotc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa