• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO
HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na maliasili
      • Raslimali watu na Utawala
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Usafi na mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Ujenzi na Uokoaji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Sekondari
      • Kilimo, Ushirika na umwagiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
    • Vitengo
      • Sheria
      • ICT and Public relations
      • Ugavi na Manunuzi
      • Mkaguzi wa ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti mbalimbali
    • Mikataba
    • Mpango Mkakati
    • Hatua
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio
    • jarida la mji

WAKULIMA LIMENI MAENEO MNAYOWEZA KUYAHUDUMIA KIUHAKIKA ILI MPATE MAZAO MENGI YENYE UBORA.

Tarehe iliyowekwa: December 7th, 2021

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Makambako,Kenneth Haule alipokuwa akijibu hoja ya Mhe. Imani Fute diwani wa kata ya Kitandililo katika mkutano wa Baraza la Madiwani,lililofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri kuhusu utoaji elimu kwa wakulima juu ya  uchaguzi wa mbolea bora kutokana na kupanda bei ya Mbolea nchini kwani matangazo ya biashara ya mbolea kwa sasa ni mengi hali inayoweza kuwachanganya wakulima.

Akijibu hoja ya kupanda bei kwa mbolea,Bw,Haule  amesema kuwa mbolea zinazotumika nchini,zinazalishwa nchi za nje na waziri mwenye dhamana ameshatoa tamko juu ya suala la bei za mbolea kupanda,lakini  licha ya kupanda bei kwa mbolea nchini,wakulima wengi wa Makambako bado wanalima kwa mazoea kwani mbolea walizozizoea kutumia ni DAP,UREA na CAN,hata wanapoelekezwa aina ya mbolea ambayo ni nzuri na inauzwa bei ya chini kuliko mbolea hizo  hawapo tayari kuzitumia.

“Katika mji wetu wa Makambako,wakulima wengi wamezoea aina tatu za mbolea DAP,UREA na CAN, na mbolea hizo kwa sasa bei zipo juu kwa mfano DAP inauzwa Tshs. 110,000 mfuko mmoja,lakini mbolea aina ya NPS inauzwa Tshs. 95,000 mfuko mmoja,lakini mkulima haoni unafuu wowote kati ya bei ya kununua DAP na NPS kwa sababu amezoea kutumia DAP,licha ya hayo yote timu ya wataalamu wa kilimo  itaendelea kutoa elimu na kuwahamasisha wakulima juu ya matumizi ya mbolea”,alisema Bw. Haule.

Aidha Bw. Haule amesema kuwa kinacho wakwamisha wakulima katika matumizi bora ya mbolea ni pamoja na kulima maeneo makubwa kuzidi uwezo wao wa kuyahudumia, kwa matarajio ya kupata mavuno mengi pasipo kutambua kuwa ukubwa wa eneo sio wingi wa mavuno,bali huduma ya mazao yaliyopo shambani.

Ametoa wito kwa wakulima kulima maeneo madogo kulingana na uwezo wa kupata pembejeo za kilimo,kama mbolea na mbegu bora ili kupata mazao mengi na yenye ubora,lakini pia matumizi ya mbolea ya samadi ili kuepukana na gharama za ununuzi wa mbolea za kiwandani,kwani samadi inapatikana kiurahisi na kwa gharama nafuu kikubwa ni kuzingatia ushauri wa wataalamu juu ya matumizi ya mbolea hiyo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako,Mhe. Salum Mlumbe amewataka watumishi wa Umma kufanya kazi kwa weledi na kuacha utoro na utovu wa nidhamu,baada ya kutangaza kumfukuza kazi mtumishi mmoja wa idara ya Afya,Frank Selestine ambaye alikua afisa muuguzi  na kumpunguzia mshahara Boniface Kyando ambaye ni Afisa mtendaji kwa kosa la utovu wa nidhamu.

Pia Mhe. Mlumbe amewasisitiza watendaji wa kata,mitaa na vijiji kukusanya mapato ya serikali kama inavyotakiwa ili kufikia lengo la ukusanyaji mapato, kwani kwa sasa makusanyo yamefikia asilimia 98.34 lengo ni kufikia asilimia 100 ya makusanyo ya mapato.

MWISHO.

Matangazo

  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 13 April 19, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 12. April 20, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 11. April 21, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 10. April 22, 2025
  • Fungua

Habari Mpya

  • Wataalamu na viongozi watakiwa kusimamia upatikanaji na utoaji wa huduma za chanjo.

    April 25, 2025
  • Makambako yang'ara katika tuzo za Afya ya Usafi wa Mazingira ngazi ya Halmashauri za Miji.

    April 09, 2025
  • Jumla ya Miti 15,000 kupandwa Halmashauri ya Mji Makambako kuelekea siku ya Miti duniani mwaka 2025.

    March 15, 2025
  • Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 2025 Mkoa wa Njombe, Mila kandamizi zaelezwa kuwa kikwazo cha ustawi na uwezeshaji

    March 09, 2025
  • Fungua

Video

Shule mpya ya Mbugani Kitandililo sekondari kupitia mradi wa SEQUIP
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Fursa za Usafirishaji
  • Orodha ya Madiwani
  • Uzalishaji wa Umeme wa Upepo
  • Organisation Structure
  • Fursa za Biashara
  • By Laws
  • Permanent Committee

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu ya Rais
  • Tovuti ya Ofisi ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Open Data Tanzania

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Makambako Town Council

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako

    Simu ya mezani: 026-2730044

    Simu ya Kiganjani: 0785635383

    Barua pepe: td@makambakotc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa