Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Afisa kilimo,Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya Mji Makambako Bi. Beatrice Tarimo,katika ufunguzi wa mafunzo kuhusu kilimo cha zao la alizeti hususani katika suala la matumizi ya Mbolea na Uchaguzi wa mbegu bora,yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri,ambapo jumla ya vikundi vitatu vimenufaika na mkopo huo.
Bi. Tarimo amesema kuwa,Nchi ya Tanzania kwa sasa inalazimika kuagiza mafuta ya alizeti nje ya Nchi,kutokana na uhaba wa zao la alizeti Nchini,kwani wakulima wengi hulima zao hilo kama ziada na kwa matumizi ya nyumbani na sio kwa ajili ya biashara.
Amesema kuwa serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji, imeona ni bora fedha zinazotumika kununua mafuta Nje ya Nchi kwa bei ghali,itolewe mikopo kwa vikundi vya wakulima wanaolima zao la alizeti ili kuwasaidia wakulima wa zao la alizeti,kulima zao hilo kwa uhakika na kwa viwango vinavyokubalika ili uzalishaji wa mafuta uwe wa kutosha.
“Halmashauri kupitia idara ya Kilimo na Maendeleo ya jamii inatoa mikopo hiyo kwa wakulima ili kuwawezesha wakulima wa zao la alizeti ambao kwa sasa uzalishaji wake ni kidogo ili waweze kuzalisha alizeti kwa wingi,lakini pia lengo la pili ni kuwainua wakulima kiuchumi ili waweze kuhudumia familia zao.Kwa sasa mikopo inayotolewa ni kiasi kidogo lakini endapo vikundi hivi vikirejesha mikopo hiyo kwa uaminifu kiwango cha mikopo hiyo kitaongezwa”, alisema Tarimo.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii, Bw. John Mwamahonje amewataka wakulima hao kutokubadili matumizi ya mikopo hiyo, na ili kufanikisha suala hilo vikundi vijitaidi kulima kwa pamoja ili kurahisisha ufuatiliaji.Kwa kikundi kitachofanya marejesho kwa uaminifu wataongezewa kiwango cha mkopo,kwani mikopo hiyo haina riba na endapo wakifanyia kazi kwa uaminifu na umakini watapata faida na kujipatia mtaji utaowawezesha kuzalisha zaidi msimu wa kilimo unaofuata.
Aidha Bw. Mwamahonje amewataka wakulima hao kuzingatia matumizi sahihi ya mbolea, kuzingatia muda sahihi wa kupanda mbegu na palizi, kusafisha shamba kwa wakati wote hadi wakati wa mavuno,kupanda mbegu kwa nafasi kwa kuzingatia vipimo vya kitaalamu. kutokupuliza dawa ya kuua magugu baada ya alizeti kuota kwani kwa kufanya hivyo mimea itateketea maana alizeti inafanana na magugu,kufukia mbolea wakati wa kukuzia ili virutubisho visipotee lakini pia kukuzia mazao wakati ardhi ina unyevu na sio wakati wa jua kali na mambo mengine ambayo yanaweza kuharibu mazao kama ambavyo wameelekezwa na wakufunzi wa mafunzo hayo Bw. Joshua ivan na Bw. Jovinatus Frednand wa makampuni ya ocp na Zambia Seed ambayo yanazalisha pembejeo za kilimo (Mbolea na Mbegu za alizeti).
MWISHO.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa