Na. Lina Sanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako, Kenneth Haule amewataka wananchi kuchangia gharama za urasimishaji kwa wakati ili zoezi likamilike kwa wakati.
Haule ametoa wito huo leo katika mkutano wa uhamasishaji wa zoezi la urasimishaji katika Mtaa wa Igangidung'u katika Kata ya Kivavi na kuwataka wananchi wote kukamilisha malipo ya utambuzi,upangaji na upimaji kwa kila kiwanja,ambapo kiwanja kimoja gharama yake ni 130,000.
Amesema kuwa, kutokana na gharama ya zoezi hilo kuwa ndogo ni vema wananchi wakachangia ndani ya muda mfupi,ili endapo miongozo ikibadilishwa kuhusu urasimishaji utekelezaji uwe unaendelea.
Flaviana Mamkwe, Msimamizi wa sekta ya ardhi katika Halmashauri ya Mji Makambako amesema kuwa, Mtaa wa Igangidung'u unakadiriwa kuwa na viwanja 860 ambavyo vitarasimishwa na kila mwananchi atafikiwa kupitia kamati ya urasimishaji ya Mtaa itayopendekezwa na wananchi.
Naye Charles Komba,Mpima ardhi katika Halmashauri ya Mji Makambako ,amewataka wananchi kutounganisha viwanja kwa kukwepa kulipa gharama ya urasimishaji kwa kila kiwanja, kwani hati itasoma kiwanja kimoja na kugawanyisha tena ni gharama .
Wananchi wa mtaa wa Igangidung'u wameunda kamati ya urasimishaji na kupendekeza juni 30,2024 kila mmoja akamilishe zoezi la uchangiaji wa gharama za urasimishaji 130,000 kwa kiwanja.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa