Na. Tanessa Lyimo
Viongozi na wataalam wametakiwa kuimarisha na kusimamia upatikanaji wa huduma za chanjo katika maeneo yao ya kiutawala,na kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapatiwa huduma ya Chanjo ili kuendeleza mapambano dhidi ya vifo vinavyosababishwa na ukosefu wa huduma hiyo.
Wito huo umetolewa leo na Mhe. Nolasko Mlowe Mwenyekiti wa Kamati ya uchumi, elimu na afya, diwani wa Kata ya Mjimwema ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa wiki ya chanjo na maadhimisho ya siku ya Malaria duniani,ambapo Kimkoa uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya kituo cha Afya Makambako.
Kaimu Mganga mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dkt.Robert Maselle amesema kuwa, Mkoa wa Njombe umefanikiwa kusimamia utoaji wa huduma za chanjo kwenye Halmashauri zote, ambapo jumla ya vituo 361 vinavyotoa huduma za afya vituo 301 vinatoa huduma ya chanjo.
Dkt. Maselle amebainisha kuwa kwa mwaka 2024,utoaji wa chanjo katika Mkoa wa Njombe ilikuwa ni asilimia 89 kati ya lengo lililowekwa na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto kupata chanjo kwa wakati sahihi, na kuhakikisha kila mtoto anapatiwa chanjo ili kuzuia mlipuko wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo katika jamii.
Jumla ya watoto 165 wenye umri chini ya miaka 5 katika Halmashauri ya Mji Makambako, wanatarajia kupata huduma ya chanjo hadi Aprili 30,2025.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa