Na. Tanessa Lyimo
Wazazi wamewataka kutowatenga watoto kwa kuhakikisha watoto wote wanapelekwa shule,ikiwa ni pamoja na wenye ulemavu na wasio na ulemavu kwani Serikali imetengeneza miundombinu wezeshi ili watoto wote wasome na kupata uelewa.
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Mji Makambako,Bi. Lilian Mwelupungwi katika maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima na elimu jumishi lililofanyika shule ya msingi Idofi katika Kata ya Mlowa akimwakilisha mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako.
Amesema lengo la Serikali katika kutengeneza miundombinu wezeshi ni kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora hivyo kutompeleka mtoto shuleni ni uchawi.
Aidha, ametoa rai kwa wazazi ,walezi na jamii kwa ujumla kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuwa walinzi dhidi ya watoto.
Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo kwa mwaka huu inasema "Ujumuishi katika elimu bila kikomo kwa Ujuzi, Ustahimilivu,Amani na Maendeleo".
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa