Na. Lina Sanga
Njombe
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Afya,Mhe. Ummy Mwalimu Mkoani Njombe,katika Mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika Viwanja vya sabasaba.
Mhe. Ummy amesema kuwa Wizara ya Afya ina deni la kupunguza gharama za kupata huduma za matibabu nchini kama ilivyofanyika kwenye mbolea,Sekta ya afya ina wajibu wakuwapunguzia mzigo watanzania wa kulipa fedha nyingi kwa ajili ya kupata huduma ya afya kwani huduma za afya ni huduma na sio biashara hivyo gharama za kumuona daktari zitashushwa.
"Kumuona daktari tu unalipa elfu kumi na tano kwa sababu gani? Mhe. Rais timu yangu tayari inafanya tathimini na tutashusha gharama za kumuona daktari ili kuwapunguzia mzigo watanzania kama ulivyotuelekeza kwa sababu afya sio biashara bali huduma,"amesema Mhe. Ummy.
Kuhusu vitambulisho vya matibabu kwa wazee wasio na uwezo,Mhe. Ummy amesema kuwa sera ya afya inasema matibabu kwa wazee wasio na uwezo ni bure,lakini kuna baadhi ya watumishi wanakiuka maelekezo na miongozo ya Serikali ya kuhakikisha wazee wasio na uwezo wanapata matibabu bure.
Ametoa agizo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote na Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wazee wasio na uwezo wanapewa vitambulisho vya matibabu bure ,na vitambulisho hivyo viheshimiwe sio mzee anapofika kwenye kituo cha afya kupata huduma aambiwe dawa hakuna wakati dawa zipo.
Pia,amesema kuwa Wizara inatambua bado wanahitaji kubeba gharama za kutoa huduma za afya ikiwemo kwa kina mama wajawazito na wanaamini bima ya afya kwa kila mtu itasaidia kuondoa changamoto ya wazee wasio na uwezo,wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kupata huduma za afya bila kikwazo cha fedha.
Mwisho amewahakikishia wana Njombe kuwa sekta ya afya itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya,watu hawatakwenda tena Mbeya,Dar es salaam au Dodoma kwa ajili ya baadhi ya vipimo na huduma za kusafisha damu zitapatikana ndani ya Mkoa wa Njombe hakutakuwa na haja ya kwenda Mbeya au Dar es salaam tena.
Mwisho ametoa wito kwa Watanzania kupata chanjo ya Uviko 19 ili kuwa salama, takwimu za kitaifa hadi jana agosti 9,jumla ya watanzania waliochanja ni Mil 15.5 wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea ambayo ni sawa na asilimia 50.53 na Mkoa wa Njombe una asilimia 46 ya watu waliopata chanjo ya Uviko 19.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa