Na. Lina Sanga
Njombe
Mwezi septemba mwaka huu Wizara ya Kilimo itakutana na wakulima wa zao la chai wa Mkoa wa Njombe na wanunuzi wote wa chai ili kupitia upya mfumo wa bei ya chai na kuzitazama upya bei ya chai.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe katika Mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika viwanja vya sabasaba Mkoani Njombe wakati akitoa salamu kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Tanzania.
Mhe. Bashe amesema kuwa chai ni moja ya mazao yaliyopata misukosuko hivyo sababu ya kupitia upya bei zipo, kwani Serikali inatoa ruzuku ya mbolea hivyo estate zote na wanunuzi wote wa chai watakua sehemu ya wanufaika wa bei ya ruzuku na gharama ya uzalishaji zitapungua.
Amesema kuwa,chai imekuwa ikiuzwa kupitia mnada wa Mombasa,Serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana na kampuni ya Mtanzania inayoitwa Bravo inaanzisha mnada wa kuuza chai unafunguliwa Dar es salaam,na magodauni yameanza kuandaliwa na mfumo wa kuuza chai umeanza na mikataba yote ya kuuza chai itasajiliwa katika soko la chai la Tanzania ili kujua bei halisi ya chai inayouzwa nje ili kutambua bei anayopata mkulima.
Aidha,amemuagiza mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka kutafuta ardhi zisizopungua jumla ya ekari 40,000,fedha zilizotolewa kwa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kufungua mashamba ya vijana, zitawekezwa Njombe na kuanzisha kituo cha kuzalisha Mbegu ukanda wa nyanda za juu kusini kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu za ngano, na maombi ya awali mil. 400 zilizotengwa kwa ajili ya kuzalisha mbegu za ukanda wa baridi yameshafanyika ili kuanza hatua ya uzalishaji mbegu.
Ameongeza kuwa mwongozo utaoongoza sekta ya parachichi umeshatengenezwa,kwa ajili ya kuongoza msimu wa parachichi, bei ya kuanzia,madaraja ya parachichi,viwango vya parachichi ili wanunuzi wanapojngia sokoni kuwe na chombo cha kuwaongoza ili kuona ushindani wa haki sokoni na mazao yanachumwa kwa viwango vinavyotakiwa.
Ametoa rai kwa wakulima kuacha kuwauzia madalali parachichi ambazo hazijakomaa kwani zinaua soko la nje,na kuwataka wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kusimamia Mwongozo utaotolewa ili parachichi zote zifungwe zikiwa zimekomaa na zimeiva ili kutouwa soko la nje.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa