• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO
HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na maliasili
      • Raslimali watu na Utawala
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Usafi na mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Ujenzi na Uokoaji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Sekondari
      • Kilimo, Ushirika na umwagiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
    • Vitengo
      • Sheria
      • ICT and Public relations
      • Ugavi na Manunuzi
      • Mkaguzi wa ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti mbalimbali
    • Mikataba
    • Mpango Mkakati
    • Hatua
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio
    • jarida la mji

Zaidi ya Mil. 264 za TASAF zatumika kujenga Kituo cha Afya Ikelu.

Tarehe iliyowekwa: December 28th, 2022

Na. Lina Sanga

Wananchi wa Kijiji cha Ikelu.Kata ya Utengule katika Halmashauri ya Mji Makambako wameishukuru Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kutoa fedha zaidi ya Mil 264, zilizotumika katika ujenzi wa majengo matatu, jengo la wagonjwa wa nje,jengo la mama na mtoto na nyumba pacha za watumishi.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Ikelu,Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Batson Nyagawa amesema kuwa,ujenzi wa Kituo hicho utawapunguzia wanachi mzigo wa gharama za matibabu kwani kwa sasa Kijiji cha Ikelu kina hospitali ya shirika la dini moja ambayo gharama za matibabu zipo juu tofauti na gharama katika hospitali na vituo vya Serikali.

Jengo la wagonjwa wa nje(OPD) na jengo la huduma ya  mama na mtoto - Kituo cha Afya Ikelu.

“Kwa sasa wananchi wengi wasio na uwezo wanalazimika kusafiri kilomita 17 kufuata huduma za afya Kituo cha afya Makambako,kwa sababu hopsitali binafsi tuliyonayo gharama za matibabu zipo juu sana tofauti na zinazotolewa Makambako kwenye kituo cha Serikali,hivyo pindi ujenzi wa Kituo hiki utakapo kamilika wananchi watapata huduma zote hapahapa,”alisema Nyagawa.

Anna Mbangala,Mkazi wa Kijiji cha Ikelu na Mjumbe wa Serikali ya Kijiji amesema kuwa,ujenzi wa kituo cha afya katika Kijiji hicho una manufaa kwa jamii hasa kina mama kwani itawapunguzia gharama ya kupata huduma za uzazi,kwani kwa sasa mama mjamzito anatakiwa kulipia gharama za kujifunga kawaida kuanzia 50,000 na 250,000 upasuaji, hali inayowalazimu kufuata huduma  hiyo Kituo cha afya Makambako kwani hakuna gharama zaidi ya kununua vifaa.

Nyumba pacha ya watumishi wa Afya Kituo cha Afya Kijiji cha Ikelu.


Mtendaji wa Kijiji cha Ikelu,Galous Myinga amesema kuwa hapo awali lengo lilikuwa kujenga Zahanati ya Kijiji kabla ya Serikali kuamuwa kujengwa kwa Kituo cha afya na walianza ujenzi wa majengo matatu ya  rasmi mwezi april,2022 kupitia michango ya wananchi ambapo kwa wakati huo walifanikiwa kukusanya jumla ya Mil 16.7 na endapo wangejenga kupitia Michango ya wananchi pekee ujenzi hadi sasa ungekuwa hatua ya Msingi.

Ametoa shukurani kwa Serikali kwa kutoa fedha zilizofanikisha ujenzi wa majengo hayo,ambayo kwa sasa yapo hatua ya ukamilishaji pamoja na kuipandisha hadhi Zahanati hiyo Kuwa Kituo cha afya.

Mratibu wa TASAF katika Halmashauri ya Mji Makambako,Neema Chaula amebainisha Kutokana na mabadiliko ya Ujenzi wa Kituo cha afya badala ya Zahanati, Serikali Kupitia TASAF inatarajia kuongeza idadi ya majengo ya kutolea huduma ikiwa ni pamoja na jengo la upasuaji,Maabara na wodi ya mama na mtoto kwa gharama ya Mil. 135.

Matangazo

  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 13 April 19, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 12. April 20, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 11. April 21, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 10. April 22, 2025
  • Fungua

Habari Mpya

  • Wataalamu na viongozi watakiwa kusimamia upatikanaji na utoaji wa huduma za chanjo.

    April 25, 2025
  • Makambako yang'ara katika tuzo za Afya ya Usafi wa Mazingira ngazi ya Halmashauri za Miji.

    April 09, 2025
  • Jumla ya Miti 15,000 kupandwa Halmashauri ya Mji Makambako kuelekea siku ya Miti duniani mwaka 2025.

    March 15, 2025
  • Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 2025 Mkoa wa Njombe, Mila kandamizi zaelezwa kuwa kikwazo cha ustawi na uwezeshaji

    March 09, 2025
  • Fungua

Video

Shule mpya ya Mbugani Kitandililo sekondari kupitia mradi wa SEQUIP
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Fursa za Usafirishaji
  • Orodha ya Madiwani
  • Uzalishaji wa Umeme wa Upepo
  • Organisation Structure
  • Fursa za Biashara
  • By Laws
  • Permanent Committee

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu ya Rais
  • Tovuti ya Ofisi ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Open Data Tanzania

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Makambako Town Council

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako

    Simu ya mezani: 026-2730044

    Simu ya Kiganjani: 0785635383

    Barua pepe: td@makambakotc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa