Na. Lina Sanga
Katibu wa NEC,Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Taifa,ndg. Paul Makonda jana alizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Mji Makambako na maeneo ya jirani ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Mkoa wa Njombe.
Akiwa katika Mkutano wa hadhara katika Halmashauri ya Mji Makambako,Ndg. Makonda amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako kuhakikisha anatekeleza maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe kuhusu mgogoro wa wafanyabiashara wa mazao kuhamia soko rasmi la mazao la Kiumba,ili kuwawezesha wafanyabiashara hao kufanya shughuli zao kwenye maeneo rasmi yaliyopangwa.
Makonda alitoa agizo hilo mara baada ya kupokea kero kwa wananchi ikiwa ni pamoja na mfanyabiashara wa mazao,kuhusu agizo la Mkuu wa Mkoa kuruhusu wafanyabiashara kufanyia wa mazao kufanyia biashara kwenye maeneo mbalimbali badala ya soko la Kiumba na wafanyabiashara wa mali mbichi kuhamia soko la Magegele na Kiumba.
Makonda amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako,Kenneth Haule kuharakisha uboreshaji wa miundombinu katika soko la Kiumba,na ifikapo Machi 15,2024 wafanyabiashara wote wahamie soko la mazao la Kiumba.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa