Na. Lina Sanga
Dar es salaam
Taarifa hiyo imetolewa na Bw. Ramadhani Kailima, Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi leo,katika kikao kazi na Maafisa habari wa Mikoa na Halmashauri nchini, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mlimani city ili kuwajengea uwezo maafisa hao ,kuongeza hamasa ili kufanikisha zoezi la uandikishaji na uchaguzi kwa ujumla.
Kailima amesema kuwa, maafisa habari wana majukumu makuu mawili ya kuwakumbusha na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha,kanuni za uboreshaji wa daftari la wapiga kura na kupinga upotoshaji unaofanyika kuhusu zoezi hilo kwa kutoa taarifa sahihi ili kujibu hoja mbalimbali za wananchi.
Bi. Giveness Aswile, Mkurugenzi wa idara ya habari na elimu ya Mpiga kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,amesema kuwa jumla ya wapiga kura wapya zaidi ya mil. 5.6 wataandikishwa ikiwa ni sawa na asilimia 18.7 ya wapiga kura mil. 29.8 waliopo kwenye daftari baada ya uboreshaji uliofanyika mwaka 2019/2020 na inakadiriwa kuwa wapiga kura kufikia mil. 34.7 baada ya uboreshaji wa mwaka huu.
Ametaja sifa za wapiga kura kuwa ni waliofikisha miaka 18 na kuendelea na wataotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu mwaka 2025 pamoja na wapiga kura waliohama Kata na Jimbo walilojiandikishia awali,wanaorekebisha taarifa na waliopoteza kadi zao.
Ameongeza kuwa jumla ya wapiga kura 594,494 wanatarajiwa kufutwa kwenye daftari la wapiga kura kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye daftari hilo ikiwa ni pamoja na waliofariki.
Ametoa rai kwa wananchi kutanguliza maslahi ya Taifa mbele kwa kutojiandikisha kwa ajili ya kupata kadi mpya, ambayo haina shida yoyote kwani utengenezaji wa kadi hizo ni gharama kubwa.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Kassim na kauli mbiu ya zoezi hilo ni "Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni Msingi wa Uchaguzi bora".
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa