Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako anapenda kuwatangazia wananchi wote kwa ujumla kwamba kutakuwa na mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Makambako ambao utafanyika tarehe 14.02.2020 katika ukumbi wa mikutano wa Lutheran Center Saa 3:00 asubuhi.
Mkutano huu utafanyika kwa lengo la kujadili Taarifa za maendeleo kila robo ya mwaka wa Fedha.
Wananchi wote mnakaribishwa kuja kushiriki kwa gharama zenu binafsi.
Ahsanteni na karibuni sana.
07.02.2020
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa