Na.Tanessa Lyimo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako Mhe.Salum Mlumbe amekabidhi hundi yenye thamani ya Mil.216.7 kwa vikundi 19 vya wanawake , Vijana na watu wenye Ulemavu ikiwa ni mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri ya Mji Makambako.

Mhe. Mlumbe akimwakilisha mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Makambako Mhe.Daniel Geofrey Chongolo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa ofisi ya Kata ya Lyamkena amewataka wanufaika kuzingatia matumizi sahihi ya fedha hizo, kama ilivyokusudiwa huku akiwasisitiza urejeshwaji wa mikopo hiyo kwa wakati ifikapo muda wa marejesho ili iweze kuwanufaisha wakopaji wengine.
Pia, amewataka wale waliokosa mkopo wa Halmashauri kuendelea kujitokeza katika taasisi za fedha ambazo Serikali imetoa mwangaza wa mikopo yenye riba nafuu ikishirikiana na taasisi hizo ikiwa ni pamoja na Benki ya NMB.

Ametoa wito kwa watu wenye ulemavu kujitokeza kwa wingi pindi fursa za mikopo zitakapojitokeza kwani mikopo hiyo ni ya jamii yoyote lengo ikiwa ni kumnyanyua mwananchi mmoja moja katika kukuwa na kumnufaisha kiuchumi.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na diwani wa Kata ya Mwembetogwa Mhe.Robert Hamis Shejamabu amewapongeza wanufaika kwa kujitokeza kuomba mikopo hiyo, huku akiwataka kuwa waaminifu na kutoruhusu hali ya ufatiliaji usio wa lazima pindi muda wa urejeshwaji wa mkopo utakapofika.

Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa