Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako anawatangazia Wananchi wote kuwa mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya tatu(Januari, Februari, March) utafanyika tarehe 12/05/2020 katika ukumbi wa Lutherani Centre mjini Makambako, hivyo wananchi wote wenye nafasi wanaruhusiwa kuhudhuria.
Mkutano wa Baraza la Madiwani hufanyika kila baada ya miezi mitatu ikiwa na lengo la kujadili taarifa za maendeleo ya Halmashauri ya Mji wa Makambako. Pia wananchi wote mnakumbushwa kuendelea kuchukua tahadhari za maambukizi ya ugonjwa wa Mapafu unaosababishwa na Virus vya Corona.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa