Na. Lina Sanga
Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Mhe. Anthony Mtaka amewataka wakazi wa Mkoa wa Njombe na wafanyabiashara kuendelea kufanya biashara bila ukomo wa muda kwani kwa sasa Njombe ipo salama na vyombo vya usalama vipo kuhakikisha amani inaendelea kutawala kama awali.

Mhe. Mtaka alitoa tamko hilo jana katika mkutano na wakazi wa Halmashauri ya Mji Makambako katika viwanja vya stendi ya zamani, na kuwataka wananchi kuendelea na maisha yao kama kawaida ikiwa ni pamoja na kufanya biashara bila kizuizi chochote.
Aidha, amevipongeza vyombo vya usalama kwa kulinda raia na mali zao zisiharibiwe kwa kuhakikisha wanazuia uharifu bila kuleta madhara kwa wananchi wasio na hatia na kuwataka wazazi na wananchi wote kukemia vitendo vya uvunjifu wa amani na ushabiki wa kisiasa usio na afya.
Pia,amewataka wafanyabiashara wakubwa kuwaelekeza vijana namna ya kuanza biashara kwa kuwaelezea mtaji wa biashara walioanza nao, hadi kukua na kumiliki biashara kubwa ambazo vijana wengi wanatamani kuzimiliki bila kujua mwanzo wake.
Baadhi ya wananchi walipata nafasi ya kutoa ushauri kwa Serikali kuhubiri na kutenda haki pamoja na kutafuta chanzo cha uvunjifu wa amani uliotokea oktoba 30,2025 na kusimamia malezi kwa wanafunzi wa chuo kwa imani ya dini pamoja na kusikiliza sauti za vijana.

Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa