Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Ndg. Paulo S. Malala, anawatangazia wananchi wote kuwa Mwenge wa Uhuru utawasili Mjini Makambako tarehe 28/05/2018 sa 2:00 asubuhi siku ya Jumatatu na kupokelewa katika kijiji cha Nyamande. Pia kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Bw. Charles Kabeho atazindua miradi 8 ya maendeleo kama ifuatavyo: Mradi wa ujenzi wa madarasa matatu shule ya msingi Mlenga, mradi wa ujenzi wa Zahanati usetule, mradi wa ujenzi wa nyumba ya muuguzi kijiji cha Manga, mradi wa kituo cha kuuza Mafuta(Sheli)-Kipagamo, mradi wa ujenzi wa mabweni mawili ya wasichana Makambako Sekondari, mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Sandarusi-Lyamkena, mradi wa ujenzi wa daraja-kata ya Kitisi, mradi wa ujenzi wa wodi ya akina mama wajawazito na watoto-hospital ya mji wa Makambako.
Hivyo wananchi wote mnaombwa kujitokeza kwa wingi, pia kutakuwa na mkesha wa Mwenge kwenye viwanja vya Polisi-Makambako ambapo tarehe 29/05/2018 mwenge utakabidhiwa halamashauri ya Wanging'ombe..
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa