Thursday 19th, September 2024
@Halmashauri ya Mji wa Makambako
Watumishi na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi hutumia Jumamosi za Mwisho wa Mwezi katika kufanya usafi ,upandaji wa miti pamoja na shughuli mbalimbali za utuzaji mazingira
Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako wakiongozwa na mkurugenzi wa Halmashauri Ndg.Paulo Sostheness Malala kwa kushiriakiana na wananchi wa Kata ya Mlowa katika kuazimisha Jumamosi ya Mwisho/Mwanzo wa Mwezi .Kuazimisha huko hufanywa takribani kila mwezi lakini mwezi huu waliamua kufanya usafi na kutunza mazingira ya eneo la hospitali Mpya ya Wilaya iliyojengwa na serikali ya awamu ya tano kupitia wizara ya TAMISEMI katika eneo la Mlowa.Wananchi wa kata ya Mlowa(ambako ndipo Hospitali ilipo) na kata za jirani wameonesha mwamko wa hali ya Juu na kufahia ushirikishwaji wao katika shughuli za kuijenga nchi yao
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa