Na. Lina Sanga
Maria Salehe Nzala mkazi wa Kijiji cha Mawande,Kata ya Utengule katika Halmashauri ya Mji Makambako ameishukuru Serikali kwa kumfadhili kupitia Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF),na kumuwezesha kumiliki nyumba.
Bi. Maria mwenye umri wa miaka 60 ambaye ni mmoja kati ya wananchama wa kikundi cha maendeleo cha TASAF katika kijiji cha Mawande, amesema hapo awali alikuwa hana nyumba na aliishi nyumba za kupanga pamoja na wajukuu wake wawili.
Amesema kuwa,mwaka 2015 kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini wa TASAF alifanikiwa kupewa mradi wa nguruwe wawili jike na dume, ambapo kupitia nguruwe hao aliweza kuwekeza kidogo kidogo kwenye kikundi cha maendeleo cha TASAF na kuanza ujenzi wa nyumba na kuendesha maisha yake pamoja na kuwasomesha wajukuu.
Aidha ameongeza kuwa, kupitia fedha anazopata kutoka TASAF kila baada ya miezi miwili ambayo ni shilingi 26,000 , inayomsaidia kupata mbolea kwa kulipa kidogo kidogo kwa wakala wa mbolea na kuwa na uhakika wa kulima.
Ametoa wito kwa wanufaika wote wa TASAF kutumia vizuri fedha wanazopewa ili kujipatia maendeleo,kwa kuanzisha na kuendeleza miradi mbalimbali ili waondokane na umasikini na kuanza maisha ya kujitegemea na kuipa nafasi Serikali kuwahudumia wengine wenye uhitaji.
Nyumba ya Bi. Maria aliyoijenga baada ya kuwezeshwa na TASAF.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa