Mhe. Salum Mlumbe,diwani wa Kata ya Lyamkena amechaguliwa leo kuwa Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya Mji Makambako kwa mwaka 2025 hadi 2030 na Mhe.Robert Shejamabu, diwani wa Kata ya Mwembetogwa amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2025/2026

Ushindi huo ni baada ya wajumbe 16 kupiga kura za ndiyo, pamoja na uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu wake,uchaguzi wa wenyeviti wa kamati kuu nne za kudumu umefanyika ambapo mwenyekiti wa Kamati ya uchumi,elimu na afya ni Mhe. Odilo Fute,Kamati ya mipango miji na mazingira ni Mhe. Nolasko Mlowe,Kamati ya kudhibiti UKIMWI ni Mhe.Robert Shejamadu na Kamati ya maadili ya madiwani ni Mhe.Rosemary Lwiva.

Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa