Na. Lina Sanga
Agizo hilo limetolewa leo na Mbunge wa jimbo la Makambako,Mhe. Deo Kasenyenda Sanga baada ya kupokea taarifa ya kukatwa kwa miti ya parachichi katika shamba la ekari tano,kutokana na mgogoro wa mpaka kati ya kijiji cha mawande kilichopo Halmashauri ya Mji Makambako na kijiji cha Banawanu kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe.
Mhe. Sanga amesema kuwa haizuiliwi mtu yeyote kumiliki shamba Wilayaau Mkoa mwingine,kwani watu wanatoka kaskazini lakini wana mashamba Njombe,hivyo huyo aliyeharibu mimea kwa kigezo cha Mpaka ana sababu zake binafsi,hivyo mtu huyo ni mharifu hivyo ni kazi ya Jeshi la polisi Kulishughulika nae kama muharifu mwingine.
“Mpaka sawa ni wa Wanging’ombe na shamba ni langu mimi kuna shida gani? huyo aliyeharibu mimea kwa kigezo na mipaka ana sababu zake binafsi kwani mimea na mpaka ni vitu viwili tofauti na havihusiani na mtu anaruhusiwa kumiliki shamba nje ya eneo analoishi”,alisema Mhe. Sanga.
Ameliagiza jeshi la polisi Makambako kushughulika na aliyeharibu mimea hiyo,na kuwataka wananchi wa Mawande kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za mtu anayeharibu mimea ili sheria ifuatwe.
Pia ametoa wito kwa viongozi kutokuwa wasababishi wa migogoro isiyokuwa na ulazima,kwa kung’ang’ania mipaka ambayo haina sababu.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa