Na. Lina Sanga
Njombe
Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji Richard Hananja,Katika Kongamano la kuiombea Nchi ya Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan,lililofanyika leo Mkoani hapa.
Hananja amesema kuwa amani ni bidhaa adimu,ustawi na utengemeno na mahali ambapo hakuna amani basi hakuna utengamano wala ustawi hata katika familia endapo amani imekosekana basi ustawi wa familia hautakuwepo.
Amesema kuwa katika nchi hii kila mtu ana nafasi yake,nafasi ya viongozi wa dini ni kuitakia amani nchi,ili nchi iendelee kustawi hivyo maombi ya leo ni kwa ajili ya ustawi wa nchi kwani amani ni maendeleo.
Ameongeza kuwa Tanzania ni ya watanzania wenyewe hivyo kuiombea nchi amani ni jukumu la kila mtanzania,ili Mungu aendelee kudumisha amani katika nchi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Nchi.
“Katika ziara ya jana ya Mkuu wa Mkoa ya kutembelea miradi tumeona miradi mikubwa nay a kupendeza,kama barabara ya zege ambayo mimi binafsi sijawahi kuiona tangu nizaliwe hadi nilitamani nilale niibusu barabara ile kabla sijafa,tukaona kiwanda cha parachichi na kiwanda cha dawa,tumeona mambo makubwa katika Nchi hii Serikali inaweza kunyamaza lakini kuna mambo makubwa yanafanyika na Mama Samia Suluhu Hassan”,alisema Mch. Hananja.
Ametoa wito kwa wananchi wote pamoja na Viongozi kusimama katika nafasi zao na kuiombea amani Nchi kwani kuna nchi zina kila kitu lakini hawana amani na watu wanaondoka na kuhama nchi zao hivyo amani ni maendeleo.
Naye Shekhe Hilal Makarani (shekhe Kipozeo),amewausia watanzania kudumisha amani na upendo bila kujali kabila wala dini,muislamu ampende mkristo,mkristo ampende muislamu,mmakonde ampende mndengeleko ili kuishi kwa amani na iwe rahisi kupata maendeleo.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa