Na. Lina Sanga
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako, Kenneth Haule mara baada ya kutembelea kaya za wanufaika wa TASAF katika Mtaa wa Idofi,Kata ya Mlowa na kuwaagiza maafisa kilimo kuhakikisha wanaandaa ratiba ya muda wa kuweka mbolea na kupiga dawa ya wadudu kwenye miti ya parachichi ili isiathiriwe na wadudu.
Haule,amesema kuwa ratiba ikiandaliwa mapema na kuwafikia kwa wakati wanufaika hao ambao wengi wao ni wazee,itawasaidia wazee hao kuweka akiba ya fedha watakazolipwa na TASAF kwa ajili ya mbolea na dawa ili kuinusuru miti hiyo ambayo baadhi inashambuliwa na wadudu kutokana na kuchelewa kupiga dawa na kukosa mbolea.
“Miti hii ya parachichi ni fedha za Serikali ambazo zilitolewa kwa wanufaika wote ili kuwajengea uchumi endelevu baada ya miaka kadhaa,hivyo kila afisa kilimo kwenye Kata na Mitaa anawajibika kuhakikisha miti hii inakuwa na inahudumiwa ili matunda yapatikane na mnufaika apate lishe na chanzo cha mapato endelevu”,alisema Haule.
Amewapongeza wanufaika wa TASAF kwa kuupokea mradi huo vizuri na kujitoa kuhudumia kwa ajili ya manufaa yao,kwani jitihada wanazofanya katika kuhudumia miti hiyo ni moja kati ya mafanikio ya Serikali katika harakati za kupunguza umasikini nchini.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa