Na. Lina Sanga
Rai hiyo imetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge,Dkt. Pindi Chana leo,katika zoezi la uzinduzi wa anwani za makazi katika Halmashauri ya Mji Makambako.
Mhe. Chana amesema kuwa anwani za makazi zinasaidia katika utambuzi wa barabara na nyumba hasa kwa wageni,lakini pia biashara ya mtandao kwani bodaboda atafikisha mzigo hadi mlangoni tofauti na sasa kwani Muda mwingi unatumika hadi kufika mahali husika.
“Ni wajibu wa kila mwananchi kushiriki katika utekelezaji wa anwani za makazi, kwani faida ni nyingi kwa Serikali na kwa kila mwananchi hasa katika biashara za mtandao na upatikanaji wa huduma za gari la wagonjwa,zimamoto na misaada mingineyo”,alisema Mhe. Chana.
Katika Halmashauri ya Mji Makambako Dkt. Pindi Chana amezindua barabara mbili,barabara ya Tanki la maji iliyopo Kata ya Makambako na Barabara ya Polisi iliyopo kata ya Mwembetogwa.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa