Na. Lina Sanga
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Mhe. Anthony Mtaka katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 2024 iliyofanyika Kimkoa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe katika Kijiji cha Usita.
Mhe. Mtaka amesema ni wakati sasa wa kufanya mabadiliko ya familia,kwa kuachana na mambo ambayo wazazi wamerithishwa kwenye kitchen party za zamani badala ya kuwafunda mabinti jinsi ya kumuhudumia mume basi wafundishwe masuala ya kukuza uchumi.
Aidha,ametoa rai kwa wanawake kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa,ili Halmashauri za Kijiji zote ziongozwe na wanawake na kutokujenga chuki dhidi ya wanawake wengine na kuhangaika kuwavuruga wanaofanya vizuri,kushiriki kumsema vibaya kwenye kikao badala yake wawape ushirikiano wataoshinda uchaguzi na kuwapongeza wanapofanya vizuri.
Pia, amewataka wanawake kuzingatia lishe bora kwa kuwafundisha vizuri mabinti,kuzingatia ulaji wa lishe kamili na wajawazito wafundishwe umuhimu wa unyonyeshaji na namna ya kujihudumia baada ya kujifungua.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa