Pichani ni Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa ,Makambako wakiwa katika Baraza la kikao cha Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako kwa lengo la kujadili agenda muhimu za Halmashauri ya Mji wa Makambako kama ifuatavyo:
- Kupitia utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani wa tarehe 17 ,02,2021
-kuwasilisha taarifa za kamati za kudumu za Halmashauri mfano, kamati ya fedha na utawala ,kamati ya mipango miji na mazingira ,kamati ya uchumi ,elimu na afya ,kamati ya kudhibiti UKIMWI ,kamati ya maadili ya waheshimiwa Madiwani ,
-kuwasilisha tuzo ya bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania (NBA ) katika ufungaji bora wa hesabu katika mamlaka za serikali za mitaa.
-ombi la kumega eneo la shule sekondari Makambako kwaajili ya kujenga shule ya Sekondari ya kata Mjimwema .
-Mapendekezo ya eneo la kujenga shule ya vipaji maalum ya kitaifa kwa wasichana wenye ufaulu mzuri
-Taarifa ya utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi kutoka mapato ya ndani kwa vikundi vya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu kwa kipindi cha kuishia mwezi decemba 2020.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa