Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe Marwa Lubilya akiwa Mgeni Rasmi wakati wa kuapishwa kwa Madiwani Kumi na sita (16) wa Halmashauri ya Mji wa Makambako uapisho ambao umefanyika mnamo tarehe 10 ya mwezi december akiwa kama mgeni Rasmi ametoa wito kwa madiwani hao kama viongozi waliochaguliwa na wananchi ni vema wakawa mstari wa mbele kutatua kero za Wananchi katika maeneo yao aidha ametaja vitu ambavyo viongozi na jamii ya Mkoa wa Njombe inapaswa kuyafanyia kazi bila kusubili nguvu ya serikali kwa Mfano suala la udumavu na utapiamlo Kwa Mkoa wa Njombe kusifika na idadi kubwa ya uzalishaji wa Mazao ya Chakula lakini ni aibu kuwa kinara katika suala la utapiamlo na uduamadu lazima jamii ibadilike ,Katika suala la Michezo ameomba wanaNjombe na jamii ya Njombe kupenda vya nyumbani kwanza maana yake kuwa na uzalendo na timu Ya nyumban akimaanisha timu ya Njombe Mji ambayo kwa sasa inaitwa Njombe sport club timu hii inachangamoto nyingi lakini wanaNjombe kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Michezo wanaweza kuifikisha timu mbali katika ligi pia amezungumzia suala la kilimo ambapo ameiasa jamii kuacha kilimo ambacho kinaweza kusababisha ukame hasa kwa wakulima wanaopenda kufanya shughuli za kilimo katika vyanzo vya Maji almaarufu kama (vinyungu ) ni bora zaidI kulima kilimo cha Matuta kwaajili ya kutunza vyanzo vya maji na kuepuka suala zima la Kuharibu vyanzo vya maji .
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa