Pichani ni kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako Appia Mayemba akizungumza na Hadhara katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako na kuhudhuriwa na Madiwani, Taasisi mbalimbali za kiserikali pamoja na wakuu wa Idara na vitengo vyake.
Lengo hasa la kikao hicho ni kujadili maendeleo ya Halmashauri ya Mji wa Makambako katika nyanja mbalimbali hususani sekta ya elimu ,Afya na miundombinu kwa ujumla wake ili kufikia malengo ya kuifanya Halmashauri kuwa mbele katika masuala mazima ya kutoa huduma kwa wananachi.
Awali Appia amezungumza kuhusu sekta ya elimu katika Halmshauri ya Mji wa Makambako amesema Jumla ya wanafunzi 2891 wanatarajia kujiunga na kidato cha kwanza januari mwakani huku kukiwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 28 kwa shule zote za sekondari, mbali na kutaja changamoto hiyo katika suala zima la kukabiliana nayo Appia ameshukuru mchango wa Mbunge wa jimbo la Makambako Deo Kasenyenda Sanga kwa mchango wake katika sekta ya elimu kwa jimbo zima la Makambako na kuwaomba Madiwani kuendelea kuhamasisha wananachi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa huku akifafanua kuwa Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022 imetenga kiasi cha shilingi Billioni ishirini na tano kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule za sekondari.
Aidha katika kuchangia maendeleo ya Halmashauri ya Mji wa Makambako diwani wa kata ya kivavi Alimwimike Sahwi amesema ili kuondokana na changamoto za upungufu wa vyumba vya madarasa kila mwaka ni vema Halmashauri ya Mji Makambako iwe na mpango kazi ambao utaenda kutatua changamoto hiyo kwa wakati muafaka ,hii itaepusha kadhia na usumbufu wa kufikri changamoto ya vyumba vya madarasa kila mwaka.
Wakati huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Hanana Mfikwa amewaomba viongozi wa taasisi mbalimbli kutoa elimu kwa wananchi watambue kuwa kadri wanavyoongezeka ndivyo wanatakiwa kutambua kuwa ni wajibu wa kuongeza vyumba vya madarasa katika maeneo yao ili kuwasaidia watoto wao sio kuiachia kila kitu serikali itatue.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa