Na. Lina Sanga
Halmashauri ya Mji Makambako hadi kufikia mwezi juni,2023 imefanikiwa kukusanya bil. 28.55 ya fedha zilizoidhinishwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023, ambapo mapato ya ndani ni bil. 2.9,ruzuku kutoka Serikali kuu bil. 21.5 na fedha za nje kwa ajili ya miradi ya maendeleo bil. 4.02.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji Makambako,Bw. Eliud Mwakibombaki katika Mkutano maaalum wa baraza la Madiwani la kupitia rasimu ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025,mapitio ya mwaka 2022/2023 na nusu mwaka 2023/2024.
Mwakibombaki amesema kuwa,katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023,Halmashauri ya Mji Makambako iliidhinishiwa jumla ya bil. 26.75 na ilipokea fedha nje ya ukomo wa bajeti uliyoidhinishwa bil. 2.32 iliyopelekea ongezeko la bajeti iliyoidhinishwa kutoka bil. 26.75 hadi bil. 28.43.
Amesema kuwa,kati ya fedha hizo zilizokusanywa jumla ya bil. 3.17 sawa na asilimia 109.93 ni mapato ya ndani, bil. 21.47 sawa na asilimia 99.76 ni fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu na bil. 3.89 sawa na asilimia 97.07 ni fedha kwa ajili ya miradi na wananchi ni mil.357.5 kati ya mil. 700.
Baraza la Madiwani limeridhishwa na taarifa ya ukusanyaji wa mapato na kuishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya madarasa na Afya.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa