Na. Lina Sanga
Rai hiyo imetolewa leo na Afisa Mwandikishaji wa jimbo la Makambako, Bw. Eliud Mwakibombaki wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa waandishi wasaidizi na waendesha BVR jimbo la Makambako, na kuwataka kuzingatia mafunzo watakayopewa na kuwasisitiza kufanya kazi kwa weledi ,bidii,kujituma na kutunza viapo vyao ili kufanikisha zoezi hilo la Kitaifa.
Mwakibombaki amesema kuwa, mafunzo hayo yanatolewa ili kuwawezesha waandishi wasaidizi na waendesha BVR kutekeleza majukumu yao katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,ambapo mafunzo hayo yatahusu ujazaji wa fomu,matumizi ya mfumo wa kuandikishia wapiga kura pamoja na matumizi sahihi ya vifaa vya uandikishaji wapiga kura.
Amewataka washiriki wa zoezi hilo ambao wamewahi kushiriki katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Tume ikiwemo ya uboreshaji wa daftari, kutumia uzoefu walionao na mafunzo watakayopata kufanikisha zoezi hilo la Tume Huru ya Uchaguzi, sambamba na kuwasaidia washiriki wengine ambao hawakuwahi kushiriki katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura lililopita.
Pia, amebainisha uwepo wa Mawakala wa vyama vya Siasa kuwepo kwenye vituo vya uandikishaji ili kuleta uwazi wa utekelezaji wa zoezi hilo na kutambua wapiga kura wa eneo husika na sio kuingilia utekelezaji wa majukumu ya maafisa uandikishaji vituoni ili kuepuka kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima.
Ametoa wito kwa washiriki wote kuhakikisha wanatumia vifaa vyote vitakavyotumika katika uboreshaji na kuzingatia maelekezo yatakayotolewa na Tume, ili waweze kuyafanyia kazi kwa usahihi katika kutekeleza zoezi la uboreshaji wa daftari na kusisitiza ushirikiano kwa watendaji wote wa uboreshaji wa daftari, watendaji wa Serikali ,vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi pamoja na watendaji wa Tume ya Uchaguzi.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa