Na. Lina Sanga
Tamko hilo limetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Mhe. Anthony Mtaka katika maadhimisho ya kilele cha siku ya mazingira duniani,ambayo katika Mkoa wa Njombe yamefanyika katika Mtaa wa Ilangamoto,Kata ya Lyamkena,Halmashauri ya Mji Makambako kwa kupanda miti 700 katika Chanzo cha maji cha Mkomela A.
Mhe. Mtaka amesema kuwa,ipo haja ya chanzo hicho cha maji kuongezewa thamani kwa kuanzisha ufugaji wa samaki aina ya kambale,ili kitumike kama chanzo cha fedha na kuongeza pato la Kikundi kinachohifadhi chanzo hicho, kwani kina sifa stahiki kwa ufugaji wa Kambale na mahitaji ya chakula yatakuwa madogo.
Ametoa rai kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako,kuanza mchakato wa kukiboresha chanzo hicho kwa kuwashirikisha maafisa uvuvi ili mradi wa ufugaji wa samaki uanze kutekelezwa,na atakabidhi vifaranga 5000 kwa ajili majaribio kwa kikundi cha Wafugaji wa Samaki cha Mkomela na kuwataka wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji kwa kutofanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji.
Pia,ametoa rai kwa wakazi wa Mkoa wa Njombe kuhamasishana kupanda miti ya matunda kwenye kaya zao ,kama vile miti ya machungwa na parachichi,ili kuondokana na magonjwa mbalimbali ikiwamo ukondefu na Kwashakoo kutokana na ukosefu wa lishe kwa watoto na kukuza kipato cha familia.
Aidha,amewataka wanufaika wa TASAF waliokabidhiwa miche ya parachichi kuhakikisha wanaendelea kuitunza na kuihudumia miche hiyo,ili baada ya miaka mitatu waanze kuvuna na kukuza kipato cha Kaya zao, na kwa mnufaika ambaye miche imekufa atatolewa TASAF.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa