Na. Lina Sanga
Agizo hilo limetolewa leo na Mhe. Zakaria Mwansasu Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe katika hafla ya uzinduzi wa upandaji Miti Kimkoa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 uliofanyika katikaSoko la mazao la Kiumba,Kata ya Lyamkena katika Halmashauri ya Mji Makambako.
Mhe. Mwansasu amesema kuwa,upandaji wa miti ni muhimu kwani miti ni chanzo cha uhai wa binadamu hivyo ni wajibu wa Halmashauri na wananchi kushirikiana kupanda miti,kutunza na kuhifadhi mazingira ili kuendelea kulinda rekodi ya Mkoa kuwa miongoni mwa Mikoa maarufu kwa kupanda miti.

Amebainisha kuwa, kwa mwaka 2025/2026 Mkoa wa Njombe una lengo la kupanda miti isiyopungua Mil 30 kwa kila Halmashauri kupanda miti Mil. 5,ikilinganishwa na mwaka 2024/2025 ambapo Mkoa wa Njombe ulipanda miti Mil. 31 na jumla ya miti Mil. 25.4 ilistawi na miti Mil. 6 haikustawi kutokana na sababu mbalimbali ikiwa kama kuliwa na mifugo pamoja na moto.

Aidha,amezitaka Mamlaka zinazohusika na uhifadhi wa mabonde kuendelea kushirikiana na Halmashauri kuweka mipaka na kuhifadhi vyanzo vya maji Pamoja na kusimamia sheria zilizopo sambamba na utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji.
Naye, Mhe. Salum Mlumbe, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Njombe kuwa Halmashauri ya Mji Makambako kwa kushirikiana na wananchi itaendelea na zoezi la upandaji miti na uhifadhi wa mazingira kwa kuzingatia faida za kuhifadhi vyanzo vya maji,upandaji miti na kuhifadhi mazingira.

Jumla ya Miti 400 imepandwa leo Katika zoezi la uzinduzi wa upandaji miti Mkoa wa Njombe.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa