Mbali na kueleza nini maana ya Saratani ya Mlango wa kizazi ,pia Mtaalam ameleza dalili za maambukizi ya HPV, Kama ifuatavyo:Baadhi ya Dalili za maambukizi ya HPV ni
-Vivimbe kwenye sehemu za uke na uume ,(au koo /haja kubwa .
-Dalili za baadae ni Mabadiliko katika seli za mlango wa kizazi ,ambazo ni Dalii za awali za Saratani ya mlango wa kizazi
-Mabadiliko haya yasipodhibitiwa mapema hugeuka kuwa Saratani ya mlango wa kizazi au viungo vingine.
DALILI ZA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
Awali Saratani ya mlango wa kizazi haina dalili hugundulika tu kwa kuchunguzwa na wataalam wa afya ,Dalili za baadae ni :
-Kutokwa na ucahfu na damu kwenye uke
-Kupata hedhi bila mapangilio maalum
-Kutokwa na Damu ukeni baada ya tendo la ndoa .
CHANJO YA KUKINGA SARATANI :
-Chanjo ya HPV inakinga Maambukizi ya virusi vya HPV vinavyisababisha Saratani ya Mlango wa kizazi .
-Chanjo ya HPV inatolewa mara mbili ili kupata kinga kamili Chanjo hii inaweza kupunguza matukio ya Saratani ya Mlango wa kizazi kwa kiwango kikubwa.
-Chanjo hii ni salama ,imethibitishwa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Shirika la Afya duniani (WHO).
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa