Na. Lina Sanga
Tamko hilo limetolewa leo na Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt Philip Mpango katika kilele cha maonesho ya nne ya Shirika la kuhudumia Vidogo (SIDO) Kitaifa ambayo kwa mwaka huu yamefanyika Mkoani Njombe.
Amesema kuwa,dhamira hiyo ya Serikali ina lengo la kuifikisha nchi kuwa nchi yenye kipato cha kati cha juu na mpango wa taifa wa maendeleo ya miaka mitano unaotekelezwa hivi sasa ,unaitaka Serikali kukuza mchango wa viwanda katika pato la taifa na ajira zinazotokana na viwanda,ambapo kwa sasa mchango wa viwanda katika pato la taifa ni asilimia 7.1 na matarajio ni kufikia asilimia 9 ifikapo mwaka 2025/2026.
Ameongeza kuwa,kupitia maonesho ya SIDO masuala mbalimbali yanayoathiri maendeleo ya viwanda vidogo yanaibuliwa ,ikiwa ni pamoja na suala la uwezo mdogo wa kuzalisha kwa wingi teknolojia mbalimbali zinazobuniwa na kusababisha kasi ndogo ya kuenea kwa teknolojia hizo, kutokana na gharama za upatikanaji wake na kuathiri maendeleo ya viwanda kwani wananchi wanashindwa kumudu gharama hizo.
Amesema ili kusambaza matumizi ya teknolojia katika uchakataji na kuongeza thamani ya mazao ni lazima kuhakikisha gharama za teknolojia,mitambo na mashine zinazozalishwa zinakuwa nafuu hivyo SIDO na taasisi zinazohusika na maendeleo ya viwanda vidogo na ubunifu kama chuo cha teknolojia Mbeya na Dar es salaam na sekta binafsi kujikita katika uzalishaji wa teknolojia rahisi zenye ubora na gharama nafuu.
Aidha,ametoa rai kwa SIDO na taasisi zingine zilizopo katika tasnia ya viwanda vidogo kubuni na kuhamasisha uzalishaji wa vifungashio bora vyenye viwango k,wa kutumia teknojia rahisi ili kuongeza thamani ya bidhaa za mazao ,kwani bidhaa nyingi zinakosa ubora na ushindani katika masoko kwa kutofungashwa vizuri.
Pia amesema kuwa,Serikali inatambua uwepo wa changamoto ya kupata mitaji kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo, hivyo taasisi za fedha zina nafasi ya kuweka masharti ya mikopo ya upendeleo kwa viwanda vidogo na kati ili kukuza uzalishaji na kuipongeza benki ya CRDB kwa kutoa mikopo kwa riba ya asilimia 9 kutoka asilimia 18 kwa viwanda vya uchakataji wa mazao kutoka.
Amelitaka Shirika la viwango Tanzania (TBS) kufanya jitihada zaidi kuwafikia na kuwasaidia wajasiriamali wadogo kupata uthibitisho wa ubora wa bidhaa zao kwa gharama nafuu na kuitaka SIDO kujiendesha kibiashara.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa