Na. Lina Sanga
Wadau wa shughuli zinazozalisha kelele katika Halmashauri ya Mji Makambako, leo wamepewa elimu ya namna bora ya kuzuia uchafuzi wa mazingira ,kwa kutumia vifaa maalumu vya kuweka uwiano wa sauti kulingana na wakati husika.
Akifungua kikao hicho , Bw. Daniel Ngalupela Afisa maliasili na Mazingira wa Halmashauri ya Mji Makambako amesema kuwa ,lengo kuu la kikao hicho ni kutoa elimu ya namna bora ya kudhibiti kelele chafuzi,ambazo zinazalishwa na baadhi ya watu kwa kutokujua viwango vya sauti vinavyokubalika kulingana na muda husika,ukaribu wa makazi ya watu,hospitali na shule.
Gift Kiwia,Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Mji Makambako amesema kuwa viwango vya sauti vinapimwa kwa kutumia vifaa maalum vya kupimia sauti,ambapo mchana sauti inatakiwa kuwa dba 60 na dba 40 usiku kwenye makazi ya watu na maeneo ya biashara dba mchana 75 na usiku dba 50,maeneo ya viwanda ni dba 85 mchana na usiku dba 65.
Ameyataja madhara ya uchafuzi wa mazingira kwa mitetemo ya sauti kuwa ni pamoja na kusababisha msongo wa mawazo, kuongezeka kwa msukumo wa damu,kuharibu maongezi au hotuba,kusababisha ukiziwi,watu kushindwa kupumzika vizuri na kuathiri umakini wa utendaji kazi.
Naye Katibu wa jimbo la T.A.G Njombe kaskazini, Mchungaji Mbaraka Njiuka, amesema kuwa ipo haja kwa Serikali kuendele kutoa elimu ya kelele chafuzi katika taasisi za dini,kwani taasisi hizo zina namna tofauti za kuabudu kulingana na maandiko ya imani zao na Katiba ya Nchi inaruhusu Uhuru wa kuabudu ambao kwa namna yoyote uzalishaji wa kelele hutokea.
Wametoa rai kwa Serikali kusaidia upatikanaji wa vifaa vya kudhibiti sauti za muziki,ili kila mdau ambaye anafanya shughuli zinazozalisha mitetemo ya sauti na kila mdau aweze kununua kwa bei rafiki wakati wowote.
Kikao hicho kimewahusisha viongozi wa dini, wauza cd na madj wanaosherehesha kwenye shughuli mbalimbali.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa