Na. Lina Sanga
Imeelezwa kuwa asilimia 20 ya Idadi ya wakulima nchini wanatumia mbolea kati ya wakulima Mil. 7 kutokana na baadhi ya wakulima kukosa elimu sahihi ya matumizi ya mbolea,ambapo kuanzia mwezi agosti 15,2022 hadi sasa zaidi ya tani 200,000 zimetumika zenye thamani ya Bil. 508.3 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo jumla ya tani 367,000 zenye thamani ya wastani wa Bil. 600 zilitumika.
Akizungumza katika kikao cha wadau wa kilimo kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Mji Hayo Waziri wa Kilimo,Mhe. Hussein Bashe ,baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoani Njombe, Bi. Rose Mayemba kuibua hoja ya fedha ya mbolea ya ruzuku kutotosheleza wakulima waliopo nchini.amesema kuwa Tanzania ina jumla ya asilimia 67 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi, ambapo katika sekta ya kilimo jumla ya kaya zinazotekeleza shughuli za kilimo ni Mil. 7 na kati ya hizo ni kaya Mil. 1.4 ndizo zinazotumia mbolea.
Amesema kuwa,baadhi ya wakulima hawaruhusu mtu yeyote kutumia mbolea katika mashamba yao ,kutokana na kukosa elimu sahihi ya matumizi ya mbolea na kupelekea idadi ya watumiaji mbolea kuwa ndogo katika baadhi ya Mikoa,ambapo Mkoa wa Njombe pekee una jumla ya wakulima waliosajiliwa kwenye daftari 190,000 na waliopata namba ya siri ya kuchukua mbolea ni 183,000 na kuanzia agosti 15,2022 hadi januari 17,2023 jumla ya tani 31,280 za mbolea zimetumika na jumla ya hekta zisizopungua 400,000 zinakadiriwa kulimwa mwaka huu.
Ameongeza kuwa,hadi kufikia sasa Mkoa wa Njombe pekee hauwezi kutumia mbolea zaidi ya tani 60,000 ,ingawa mbolea ya ruzuku imehamasisha wakulima wengi kulima mazao tofauti na mwaka jana,ambapo kwa mwaka 2022 jumla ya hekta 351,000 zililimwa na jumla ya tani 49,000 za mbolea zilitumika.
Ametoa wito kwa Halmashauri kutambua vituo ambavyo vitasajiliwa kwa mtindo wa NFRA kulingana na mgawanyiko wa wakulima wake,kwa sababu mfumo wa mbolea ya ruzuku unaruhusu kuuza mbolea kwenye maeneo yaliyosajiwa pekee,hivyo kukosekana kwa mawakala kwenye maeneo wanayopatikana wakulima imekuwa changamoto hali inayomlazimu mkulima kusafiri umbali mrefu kufuata mbolea.
Katika Halmashauri ya Mji Makambako Jumla ya wakulima 19,451 walisajiliwa kwenye daftari kwa ajili ya kupata mbolea ya ruzuku,wakulima 18,026 wamesajiliwa kwenye mfumo na kupata namba ya siri ya kuchukua mbolea na jumla ya tani 1,393. 53 zenye thamani ya Bil. 1.5 zimesambazwa kwa wakulima.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa