Na. Lina Sanga
Rai hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa , Ndg. Balozi Emmanuel Nchimbi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa stendi ya zamani katika Halmashauri ya Mji Makambako.
Nchimbi alisema kuwa,ipo haja kwa wananchi na viongozi wa Serikali kuwa wazalendo wa Nchi yao, kwa kufanya kazi kwa uaminifu kwa maslahi ya Umma kwa kutoiba na Vyombo vinavyohusika kuhakikisha vinazuia wizi kwa kufanya upelelezi wa kutambua viashiria vya utekelezaji wa uhalifu na kuzuia kabla haujatekelezwa.
Alitoa rai kwa wananchi kuwa wazalendo kwa kutofanya mambo yasiyojenga Nchi , kwa kufanya kazi mahali walipo kwa uaminifu ,kwani Tanzania bado ni Nchi changa na inajengwa na watanzania wenyewe wakiamua kwa kufanya mambo ya kuijenga Nchi badala ya kuiba na kuhujumu miradi kwa kutengeneza vitendea kazi visivyo na ubora kama kalvati isiyo na nondo.
Aidha aliitaka TAKUKURU kuhakikisha inafuatilia miradi mikubwa ya maendeleo tangu inapoanza hadi kukamilika, kwa kuhakikisha fedha ya Umma inatumika vizuri na hakuna fedha ya Umma inayoibiwa.
Pia , aliwataka wananchi wa Mkoa wa Njombe kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa kutambua kuwa, Njombe ni moja kati ya Mikoa mitano inayoilisha Nchi kwa miaka zaidi ya ishirini hivyo Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kuisisitiza Serikali kuendelea kuhakikisha zana za kilimo zinapatikana kwa wakati zikiwa na ubora unaostahili na kuwakataa mazimwi wanaokula njama ya kupunguza ubora kwa maslahi binafsi.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa