Na. Lina Sanga
Tanga
Kutokana na kukosekana kwa taarifa za uwepo wa vivutio vya utalii katika baadhi ya mikoa Nchini,na kupelekea Serikali kukosa mapato katika sekta ya utalii na baadhi ya nchi kutambulisha vivutio hivyo kama vyao, filamu ya Royal Tour inafungua milango ya Kuitambulisha dunia kuhusu Vivutio vinavyopatikana nchini Tanzania ili kuongeza mapato kwa kuongeza idadi ya watalii.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kuitangaza Tanzania kupitia Royal Tour, Dkt, Hassan Abbas,Katika Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali Mkoani Tanga.
Dkt. Abbas amesema kuwa filamu ya Royal katika nchi yoyote duniani Mhusika mkuu ni Rais aliyepo madarakani, hivyo Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilimlazimu kusimama katika nafasi hiyo kwa nafasi yake na sio wasanii wengine wa filamu za bongo wala mchezaji maarufu.
Aidha, amesema katika uzinduzi uliofanywa nchini Marekani ambako ni soko kuu la utalii wa Tanzania,ameweza kukutana na viongozi matajiri namba moja katika sekta mbalimbali ambao wameonyesha nia ya kuwekeza hapa nchini.
Ameongeza kuwa filamu hiyo ya kihistoria, imetengenezwa katika kiwango cha kimataifa na wataalam nguli duniani, ambao pia wana mitandao mikubwa ya kuisambaza na inaweza kutazamwa na watu zaidi ya bilioni moja ndani ya muda mfupi.
Pia amempongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa aliyofanya,na kuwaomba maafisa Habari na watanzania kwa ujumla kumwombea katika kazi kubwa anayoifanya,ya kuitangaza na kuifungua Tanzania duniani ili kuvuta wawekezaji na watalii nchini.
Mwisho Dkt. Abbasi ametoa wito kwa Maafisa Habari kuitangaza filamu ya Royal Tour ili wananchi watambue Serikali ipo kazini na kumkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa nakala ya filamu hiyo ili isambazwe nchini kupitia kwa maafisa hao.
Kauli mbiu ya kikao hicho ni "Mawasiliano ya Kimkakati nyenzo muhimu kufanikisha sensa ya Watu na Makazi 2022".
#jiandae kuhesabiwa
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa