Pichani ni gari Jipya la Halmashauri ya Mji wa Makambako , Gari ambalo limenunuliwa kwa gharama ya shilling million mia moja sabini na mbili ,kwa kutumia mapato ya ndani ,Gari hili limenunuliwa kwa lengo la kubeba taka katika Mji wa Makambako nia ni kuweka Mji katika hali ya usafi kwani gari hili litakuwa na ratiba ya kupita katika maeneo ya vizimba na sehemu ambazo zitakuwa na taka zilizokusanywa na Wananchi .Mnamo tarehe 26/02/2021 gari hili limezinduliwa rasmi na Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri na kuanza rasmi kwa kazi ya kubeba taka katika Halmashauri ya Mji wa Makambako .
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa