Na. Lina Sanga
Hayo yamebainishwa na baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Makambako,katika Mkutano wa baraza la Madiwani la kuishia kipindi cha robo ya tatu(Januari – Machi) 2022/2023 lililofanyika juni 6,mwaka huu.
Mhe. Imani Fute,diwani wa Kata ya Kitandililo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi,Elimu na Afya amesema kuwa kutokana na ongezeko la wanafunzi wanaohitimu masomo ya kidato cha nne,Halmashauri kupitia Kamati hiyo imeona ipo haja ya kuanzisha shule za kidato cha tano na sita kwa wingi ili kutoa fursa kwa wanafunzi wanaohitimu masomo ya kidato cha nne kuendelea na masomo.
Amesema kuwa, mchakato wa shule ya Maguvani kuwa na kidato cha tano na sita unaendelea na kutoa rai kwa Halmashauri kupitia idara ya elimu sekondari,kuhakikisha mchakato unakamilika mapema ili mwezi julai shule hiyo ianze kufundisha masomo ya kidato cha tano na sita.
Aidha, ameongeza kuwa mchakato wa shule ya sekondari Mlowa kuwa ya wasichana pekee unaendelea,na kwa mwaka huu kidato cha kwanza kuna wanafunzi wa kike pekee.
Pia,katika mkutano huo wa baraza la Madiwani walimu wa shule za sekondari za Serikali na binafsi walipongezwa kwa kupewa zawadi kwa shule zilizoongoza kwa kila somo katika mitihani ya kidato cha pili na kidato cha nne 2022,ambapo shule ya Sekondari Emmaberg,Kitandililo,Kerith na Naboti zimeibuka vinara kwenye masomo mengi zikifuatiwa na shule ya Sekondari MCF,Deosanga,Maguvani na Makambako.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa