Na. Lina Sanga
Halmashauri ya Mji Makambako imeibuka mshindi wa jumla katika mashindano ya UMITASHUMTA 2022 baada ya kufanya vizuri katika michezo ya riadha ya kawaida,mpira wa pete,riadha maalumu,goal ball na fani za ndani
Hayo yameelezwa na Afisa utamaduni wa Halmashauri ya Mji Makambako,Ester Mwakalindile katika mkutano wa baraza la madiwani la robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2021/2022,lililofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji Makambako.
Mwakalindile amesema kuwa ushindi huo umepelekea Halmashauri ya Mji Makambako kutwaa jumla ya vikombe sita na medali sita, na jumla ya wanafunzi ishirini kutoka Makanbako wameungana na wanafunzi wa Halmashauri zingine kuunda timu ya Mkoa itayoshiriki mashindano ya UMITASHUMITA ngazi ya taifa mkoani Tabora agosti 30 hadi agosti 8,2022.
Akipokea vikombe na medali kutoka kwa wanafunzi hao,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako,Mhe. Hanana Mfikwa amewapongeza walimu wa michezo na wanafunzi kwa ushiriki mzuri wenye tija katika michezo na kuiwakilisha vizuri Halmashauri ya Mji Makambako na kuwakabidhi fedha kiasi cha shilingi laki moja kama zawadi.
#jiandaekuhesabiwa2022
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa