Na. Lina Sanga
Dar es salaam
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe. Nape Nnauye leo Mbele ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Kikao kazi cha 18 cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kinachofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
Mhe. Nape amesema kama Msemaji Mkuu wa Serikali,Gerson Msigwa anaingia kwenye baraza la Mawaziri hivyo hakuna sababu ya Maafisa habari ngazi za Mikoa,Wilaya na Halmashauri kutoingia kwenye vikao vyote vya maamuzi kwani wanabeba taswira ya taasisi.
Amesema kuwa,ili kuboresha sekta ya habari nchini,Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inaandaa mkakati wa mawasiliano ambao utafanya mapinduzi makubwa katika sekta ya habari na Mawasiliano ikiwa ni pamoja na kuboresha mawasiliano baina ya Serikali na Umma kwa kuzingatia namna bora Serikali inavyowasiliana na Umma lakini pia Umma unavyowasiliana na Serikali.
Aidha,amebainisha changamoto mbalimbali zinazovikabili vitengo vya Mawasiliano Serikalini ikiwa ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kisasa,upungufu wa Maafisa habari na kasi ya Mitandao ya kijamii katika kuhabarisha Umma.
Ametoa Wito kwa Wizara na Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa nchini kutenga fedha kwa ajili ya vitengo vya habari na kuongeza ajira za Maafisa habari.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa