Na. Lina Sanga
Mkuu wa wilaya ya Njombe,Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa amewapongeza Wananchi wa Kijiji cha Kifumbe katika Kata ya Mahongole,kwa Kuchangia jumla ya shilingi mil.36 zilizotumika katika ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi kifumbe,ambapo ujenzi wa darasa moja la wanafunzi wa awali limekamilika na linatumika likiwa na zana rafiki za kufundishia na kujifunzia.
Mhe. Kasongwa ametoa pongezi hizo leo baada ya kukagua ujenzi wa madarasa hayo,ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kijiji kwa kijiji,mtaa kwa mtaa iliyoanza rasmi leo katika kijiji cha Kifumbe na Usetule,Kata ya Mahongole katika Halmashauri ya Mji Makambako.
“Niwapongeze Wananchi wa Kifumbe kwa kujitoa kwenu na kufanikisha ujenzi wa madarasa haya,hasa hili darasa la wanafunzi wa awali kwa kweli mmefanya vizuri sana,nimeridhishwa na viwango vya darasa hili lakini pia zana za kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi hongereni sana”,alisema Mhe. Kasongwa.
Akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa madarasa hayo Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kifumbe, Mwl. Robert Mgulwa amesema kuwa jumla kuu ya Ujenzi wa madarasa matatu hadi sasa ni shilingi mil 48.5,ambapo Mchango wa Serikali ni shilingi Mil 12.5 na Michango ya wananchi ni Mil 36,madarasa mawili yapo katika hatua ya Ukamilishaji na darasa moja la wanafunzi wa awali limekamilika na linatumika.
Pia Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya amezungumza na wananchi wa kijiji cha Kifumbe na Usetule na kusikiliza kero zao sambamba na kutoa elimu ya Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23,mwaka huu,Mbolea ya ruzuku na Chanjo ya Uviko 19.
#Jiandaekuhesabiwa2022
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa