Na. Lina Sanga
Wizara ya Mambo ya ndani inatarajia kutoa fidia kwa wakazi 14 katika mtaa wa Lumumba,Kata ya Mwembetogwa katika Halmashauri ya Mji Makambako ikiwa ni baada ya tathimini ya awamu ya pili kukamilika.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani,Mhandisi Hamad Masauni baada ya ombi la Mhe. Deo Kasenyenda Sanga kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza na wakazi wa Mji wa Makambako leo,baada ya zoezi hilo la ulipaji fidia kuchukua muda mrefu kukamilika na kupelekea wananchi kuishi mazingira duni baada ya kuzuiwa kuendeleza ujenzi wa nyumba zao.
Mhe. Masauni amesema kuwa,uthamini wa awali ulipofanyika wananchi hao walitakiwa kulipwa fidia ya mil. 89 na wananchi hao waligoma kupokea fidia hiyo,kwani tathimini hiyo ilihusisha shughuli ambazo wamezifanya za kimaendeleo na sio ardhi.
Ameongeza kuwa,baada ya kupokea maelekezo ya kurudiwa kwa tathimini hiyo kutoka kwa Rais,tathimini hiyo ilirudiwa kwa kuhusisha ardhi na kufikia jumla ya shilingi Mil. 209 ambazo zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka 2022/2023 ambazo zitalipwa wakati wowote kuanzia sasa.
Ametoa wito kwa wananchi kutokuwa na wasiwasi kwani Waziri wa Fedha amethibitisha kuwa,fedha hizo ni miongoni mwa fedha zitakazolipwa katika mwaka huu wa fedha.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa