Kamati ya Fedha na Uongozi ikiongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Mhe. Hanana Mfikwa yafanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo 18/07/2019, miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Makambako kata ya Mlowa, ujenzi wa Zahanati ya Ibatu kata ya Kitandililo, Ujenzi wa nyumba 2 za walimu na jengo la utawala shule ya sekondari Mlowa kata ya Mlowa, ujenzi wa darasa 1 shule ya msingi Kihanga kata ya Mlowa, ujenzi wa Vyoo matundu 16 shule ya msingi Juhudi kata ya Makambako, ujenzi wa madarasa 2 shule ya msingi Kahawa kata ya Kitisi, ujenzi wa kituo cha abiria stendi kuu Makambako kata ya Kitisi, na ujenzi wa madarasa 7 shule ya sekondari Lyamkena kata ya Lyamkena.
Katika ziara hiyo, waheshimiwa madiwani walipongeza baadhi ya miradi kutokana na maendeleo mazuri, pia walitoa kasoro baadhi ya miradi na kutoa ushauri mzuri nini kifanyike ile miradi hiyo ikamilike vizuri na kwa wakati.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa