Na. Lina Sanga
Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya Mji Makambako imempongeza Bw. Anthony Mdekwa,mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kwa kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa Mradi wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa shule z awali na msingi(BOOST) akiwa moja kati ya wajumbe wa kamati ya ujenzi shule ya msingi Uhuru.
Pongezi hizo zimetolewa leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako,Mhe. Hanana Mfikwa pamoja na wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi,katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha kuishia robo ya nne (aprili – juni) 2022/2023.
Mhe. Hanana amesema kuwa uwepo wa wananchi mbalimbali kutoka vyama tofauti vya siasa ni kiashiria cha ukomavu wa siasa nchini,kwa kutambua kuwa maendeleo hayana chama na kujitoa kuhakikisha fedha zilizotolewa na Serikali zinatumia kwa lengo lililokusudiwa.
Ametoa wito kwa wananchi kujitoa kushiriki shughuli mbalimbali katika miradi ya maendeleo inayopokea fedha kutoka Serikalini ili fedha zitoshe na kukamilisha miradi ,pamoja na kuimiliki miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao kwa kusimamia kwa ukaribu ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kutokuwepo kwa ubadhirifu wowote.
Halmashauri ya Mji Makambako ilipokea Mil. 1.171 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa,ofisi,jengo la utawala na matundu ya vyoo katika shule sita ambazo ni shule ya msingi Mshikamano, Uhuru, Umoja, Juhudi,Azimio na Magegele.
Shule ya Msingi Mshikamano madarasa 6 na matundu 3 ya vyoo,Uhuru madarasa 6 na matundu 3 ya vyoo,Umoja madarasa 5 na matundu 3 ya vyoo,Juhudi madarasa 8 na matundu 6 ya vyoo, Magegele ujenzi wa madarasa 6 na matundu 6 ya vyoo na Azimio ujenzi wa shule mpya yenye mkondo mmoja wenye madarasa 7,jengo la utawala 1,matundu 10 ya vyoo,madarasa 2 na matundu ya vyoo 6 ya mfano kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la awali pamoja na kichomea taka.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa