Na. Lina Sanga
Uwepo wa madaktari bingwa wa Rais Samia umeelezwa kuleta nafuu kwa wananchi wenye matatizo mbalimbali ya kiafya, kwa kupata huduma karibu na makazi yao badala ya kufuata huduma za kibingwa kwenye hospitali kubwa nje ya Mji wa Makambako.
Hayo yameelezwa na Prince Mchwao moja kati ya wananchi waliofika kupata huduma za kibingwa leo katika hospitali ya Mji wa Makambako iliyopo Kata ya Mlowa,ambapo madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na ukunga,magonjwa ya ndani,magonjwa ya Watoto na Watoto wachanga na magonjwa ya kinywa na meno ameweka kambi kwa siku tano kuanzia septemba 22 hadi 26,2025.
Awali, Dkt. Paul Katenda ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama na uzazi amethibitisha kuwa, wanawake wengi wana shida kubwa ya maambukizi kwenye via vya uzazi(PID) na uvimbe kwenye via vya uzazi ambavyo vinaweza kusababisha ugumba na kutoa wito kwa kina mama kufanya uchunguzi mapema ili waweze kupata matibabu mapema pamoja na kutumia kinga wakati wa kujamiiana Ili kuepuka maambukizi ya PID.
Dkt. Ally Senga,Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo amesema kuwa Magonjwa ya ndani kama presha na kisukari na magonjwa ya uzazi kwa kina mama kama uvimbe kwenye kizazi na magonjwa mengine yanayosababisha ugumba na utasa ni baadhi ya magonjwa ambayo watu wengi wamejitokeza kutibiwa huku akielezea mfumo wa Maisha kuwa chanzo cha magonjwa hayo.
Jumla ya wagonjwa 248 wamepata huduma ya Afya katika kambi ya madaktari bingwa awamu ya nne katika Halmashauri ya Mji Makambako ambayo itahitimishwa kesho Ijumaa septemba 26,2025
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa