Pichani ni viongozi mbalimbali waliohudhuria katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa MakambAko katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako ,:Wageni meza kuu ni pamoja na, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Paulo Malala ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Ndg Hanana Mfikwa ,Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Makambako salum Mlumbe na katibu tawala wa wilaya ya Njombe Ndg Emanuel George ,katika Baraza hilo katibu tawala wilaya ya Njombe amezungumzia suala la ununuzi wa gari uliofanywa na Halmshauri ya Mji wa Makambako ,ununuzi wa gari la kubeba taka ambalo limenunuliwa kwa gharama ya shilingi million sabini na mbili ambapo ameshauri kama kuna uwezo wa kunua gari la pili basi iwe hivo kutokana na uhitaji hasa wa kuifanya Makambako kuwa safi na salama ,Pia zoezi la wazazi kuchangia chakula shule ambapo amewaomba Madiwani ,Watendaji kujitoa hasa katika suala la kuhamasisha wazazi kutoa michango ya chakula kwa watoto wao mashuleni kwa lengo la kuwasidia watoto kupata chakula pindi wanapokuwa shule , Pia amezungumza suala la watendaji kufauta sheria za nchi na mamalaka husuka hasa katika suala zima la usalama ,wafanye kazi za kuwatumikia wananchi kwa umakini na weledi mkubwa sambamba na kusimamia zoezi la ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwa wakati .
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa