Na.Lina Sanga
Mbunge wa jimbo la Makambako, Mhe. Deo Kasenyenda Sanga ameagiza mamlaka ya kijiji cha ikelu kuanza majadiliano ya kukipandisha hadhi kijiji hicho kiwe Kata kwani kina sifa ya kuwa Kata na kuwa na mitaa badala ya vijiji.
Agizo hilo limetolewa leo na Mhe. Sanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi ya kijiji cha Ikelu,baada ya mwananchi kumuomba Mbunge kuwasaidia kijiji chao kiwe Kata kamili kwani kina vijiji vitano ambavyo navyo vina hadhi ya kuwa mitaa.
Mhe. Sanga amesema kuwa kijiji cha ikelu kina vigezo vyote vya kuwa Kata kwani huduma zote muhimu kwa wananchi zipo,kama shule na hospitali na sasa kituo cha afya kinajengwa hivyo mchakato wa kujadiliwa kuwa Kata uanze mara moja.
Ametoa wito kwa wananchi wote wa Kijiji cha ikelu kushiriki kikamilifu kazitia zoezi la Sensa ya watu na Makazi Agosti 23 mwaka huu,ili idadi kamili ya watu wanaoishi kijijini hapo ipatikane,lakini pia idadi ya makazi ijulikane kwani kigezo kikubwa cha kupata Kata ni idadi ya watu.
Aidha,ametoa rai kwa wananchi wote ambao hawajapata chanjo ya Uviko 19 kujitahidi kuchanja,kwani chanjo hiyo haina madhara yoyote kwenye mwili wa binadamu zaidi inaongeza kinga ya kupambana na kirusi cha korona.
Pia, Mhe. Sanga ameunga juhudi za maendeleo zinazofanywa na wananchi katika ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa kuchangia bati 50 kwa ajili ya shule shikizi ya Ikelu B, mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa madarasa mawili shule ya Msingi Ikelu, mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi,pamoja na jezi na mpira mmoja kwa vijana wa kijiji hicho ili kuwawezesha kushiriki michezo na kukuza vipaji vyao.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa